• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Serikali Kuajiri Walimu 2000 Wa Masomo ya Sayansi: Naibu Waziri Kakunda

Posted on: August 4th, 2018


Serikali Kuajiri Walimu 2000 wa Masomo ya Sayansi : Naibu waziri Kakunda

Naibu Waziri Ofisi ya Rais (OR-TAMISEMI) Mhe Joseph Kakunda, amesema serikali ipo katika hatua a mwisho kukamilisha mchakato wa kuajiri waalimu 2000 wa masomo yasayansi ili kupunguza changamoto ya uchache wa walimu wa kada hiyo katika shule za umma nchini

Mhe. Kakunda ameyasema hayo katika shule kongwe ya Sekondari Mdabulo, akiwa kwenye ziara ya kikazi Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya Mkuu wa shule hiyo  Bw. George Mgomba, kueleza changamoto ya uhaba wa walimu wa sayansi katika shule yake.

 “Serikali kwa mwaka huu inaendelea na mchakato wa kuajiri walimu wa sayansi wapatao 2000 hivyo, taarifa yenu naichukua mwenyewe na kuipeleka kwa Mhe. Waziri Jafo, bila shaka walimu wawili 02 mnaowahitaji katika shule yenu mtawapata na  hili nalibeba kwa ajili ya utekelezaji”  alisisitiza Waziri Kakunda

Aidha, Mhe. Kakunda ameridhishwa na majengo mapya  ya Shule hiyo iliyojengwa kwa mfumo wa “Force Account”  kwa kuzingatia maelekezo ya kitaifa baada ya kujionea madarasa na mabweni mazuri hivyo, amesisitiza utaratibu uliotumika wa kujenga kwa njia ya Force Account uendeleee hata wakati wa mradi wa ujenzi wa mabweni utakapoanza, ambapo serikali tayari imetenga Jumla ya Tsh Milioni 100 kwa shule ya Sekondari Mdabulo.

Kwa mujibu wa mkuu wa shule ya Sekondari Mdabulo Mwalimu George Mgomba, ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuwapatia zaidi ya Tsh milioni 250 kwa ajili ya upanuzi wa miundo mbinu ikiwemo ujenzi wa vyumba 04 vya madarasa kwa gharama ya Tsh milioni 80, ujenzi wa mabweni 02 yaliyogharimu Tsh milioni 150, Ujenzi wa vyoo Tsh milioni 11 na kuimarisha maabara kwa gharama ya Tsh Milioni 18.

“Aidha, napenda kuwashukuru wadau waliosaidia na kutuchangia kukamilisha ujenzi kwa wakati, ambao ni bodi ya shule, ambao ilichangia msitu kwa ajili ya mbao, Rural Development Organization (R. D. O) ambao walitoa mashine za kuchanganya zege kwa siku 30 bila malipo na kampuni ya china Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC) walitoa malori ambayo yalibeba tripu 12 za mchanga bila malipo,  majengo hayo kwa sasa yanatumika toka Agosti 2017”

Shule kongwe ya Sekondari Mdabulo ilianzishwa rasmi mwaka 1984 ikiwa ni moja kati ya shule za wananchi wa Wilaya Mufindi, mwaka 1986 ilisajiliwa ikiwa miongoni mwa shule zinazomilikiwa na Mufindi Education Trust (MET), mwaka 2003 shule ilikabidhiwa rasmi Serikalini kufuatia sera ya serikali ya kila Kata kuwa na Shule ya Sekondari, tangu mwaka huo mpaka sasa Shule imeendelea kujengwa na wananchi, wadau mbalimbali, Halmashauri ya Wilaya na Serikali kuu .

Shule ya Sekondari Mdabulo ipo katika Wilaya ya Mufindi, Tarafa ya Ifwagi, Kata ya Mdabulo katika Kijiji cha Kidete umbali wa kilometa 45 kutoka makao makuu ya Wilaya Mufindi.

.



Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.