• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Historia

 

                         HISTORIA YA WILAYA YA MUFINDI

Mwaka 1961 wakati tunapata uhuru Tanganyika au Tanzania Bara ilikuwa na majimbo tisa na Wilaya ya Mufindi ya Sasa ilikuwa ni moja ya eneo katika jimbo la Nyanda za juu Kusini (Iringa, Ruvuma na Rukwa ) maeneo mengine ambayo leo ni ya Wilaya inayojitegemea  ni  Njombe na Iringa .

Kabla ya Tanganyika kupata Uhuru, Wilaya ya Mufindi ya sasa ilikuwa chini ya Wilaya ya Iringa. Wakati huo Iringa iliitwa Uhehe “Native Authority” chini ya Mtawala Mtemi aliyeitwa (Mutwa) Adam Sapi Mkwawa( Mkwavinyika yaani  “Mtawala wa maeneo” .

Wilaya ya Mufindi baada ya Uhuru

Baada ya Uhuru 1961 Ofisi ya Bwana Shauri Mkuu wa Wilaya iliendelea kuwa eneo la kibao na aliendelea kuwepo, bwana Shauri Cyprian Lutu. Aidha, eneo hilo la kibao lilikuwa pia na kituo cha Polisi 

Mabadiliko ya Utawala

Mwaka 1963 Serikali ya Tanganyiaka ilifanya mabadiliko makubwa ili kuondoa Utawala uliokuwepo wakati wa ukoloni, badiliko hilo liliondoa sera ya Uchifu na kuweka Tarafa “Division Executive Officers” ambao waliitwa Makatibu Tarafa          Sasa wanaitwa maafisa Tarafa, eneo lililokuwa na utawala chini ya Wanzagila na badaye “Division Executive Officers” maeneo hayo ni pamoja na Ifwagi, Kibengu, Malangali, Sadani na Kasanga ambazo kwa sasa ni miongoni mwa kata 27 za Halmashauri.

Aidha, Mabadiliko haya yalikuwa hayajaeleweka Vizuri kwa wananchi wa kawaida  kwa kuwa walikuwa wamezoea utawala wa kichifu, ambapo, kwa asili ni baadhi ya koo fulani tu ndiyo zilikuwa na sifa za kutawala, hali hii ilisababisha wale wote walioteuliwa kuchukua nafasi za Machifu wapate vitisho kutoka kwa Machifu  na  wananchi kwa ujumla.

Kwa Wilaya ya Mufindi, Mutwa Adam Sapi Mkwawa, alipita yeye mwenyewe maeneo yote akitoa elimu juu ya mabadiliko hayo, utaratibu alioutumia ulikuwa, kufanya Vikao vya ndani na wasaidizi wake. Pili mikutano ya hadhara kwa wananchi wote. Hii ilisababisha eneo la Iringa (uhehe) kutokuwa na tatizo kubwa kutokana na mabadiliko yaliyotokea

Baadhi ya “Sub – Chief’s (wanzagila) walipewa nafasi ya kuendelea kutawala kwa Division ya Executive Officers’ lakini walibadilishwa vituo vya kazi ili uchifu usiendelee pamoja na uhamisho huo walipatiwa mwongozo wa kuendesha shughuli za kiutawala Mwongozo huo ulikuwa  ni pamoja na kusimamia mkusanyiko wa kodi, shughuli za Maendeleo pamaoja na masuala ya ulinzi na usalama ( Uhakimu/ kuamua kesi)

Kuanzishwa kwa Wilaya ya Mufindi

Tarehe 01/10/1965 Wialaya ya Mufindi ilizinduliwa rasmi na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere, na Mkuu wa Wilaya wa Kwanza aliitwa Fred Mwakamyanda, wakati huo Mkuu wa Wilaya alifahamika kama “Area Commissioner” na Makao makuu ya Wilaya yalikuwa katika eneo la kibao.

Asili ya Jina Mufindi

Jina MUFINDI, lilitokamna na jina la Mti unaoitwa Mfinza kwa Lugha ya Kihehe uliopatiakana eneo la Ihomasa. Aidha, Wajerumani wailiofika kwa mara ya kwanza walishindwa kutamka neno Mfinza na badala yake wakawa wanatamka mfindi. baada ya mazoea ya Muda mrefu neno Mufindi likazaliwa.

Mkuu wa Wilaya “Area Commissioner” walikuwepo toka kuanzishwa kwa Wilaya hadi hivi sasa (1965 – 2018) ni kama inavyoonyeshwa hapa chini.

Wahe. Wakuu wa Wilaya 1965 - 2018

Na
        MWAKA
             JINA
   JINSI
01
1965 - 1971
Fred       Mwakamyanda
     Me
02
1971 - 1973
Hosea Mbembele
     Me
03
1973 - 1976
Edward Mnyawami
     Me
04
1976 - 1987
Bernad Mkusa
     Me
05
1987 - 1990
Col. Edmundi Mahawa
     Me
06
1990 -1996
Mathew Sedoyeka
     Me
07
1996 -1998
Juma Maulid Kago
     Me
08
1998 - 2006
Pascal T. Mhongele
     Me
09
2006- 2015
Evarista N. Kalalu
     Ke
10
2015 - 2015
Mboni    Mhita
     Ke
11
2015 -2016
 Jowika   Kasunga
     Me
12
2016 – Mpaka Sasa
Jamhuri  D. William
     Me

 

Kuzaliwa Kwa Halmashauri ya Mufindi

Mwaka 1974, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ilianzishwa rasmi ikiwa bado na utegemezi Mkubwa wa maamuzi kutoka Serikali kuu na makao makuu yake yalikuwa eneo la Kibao.

Mwaka 1975 makao makuu ya Wilaya na Halmashauri yalihamishwa kutoka Kibao kuja Mafinga wakati huo Mji wa Mafinga ulifahamika kama John’s Corner.

Wahe. Wenyeviti wa Halmashauri 1985 - 2018

 
     Mwaka 
     Jina
         Jinsi
01
1985 - 1990
Mhe. M. Mtengela
          Me
02
1990 -1994
Mhe. A.A Kikalao
          Me
03
1994 -2005
Mhe. Tasil M. Mgoda
          Me
04
2005-2010
Mhe. Naucerd Nyaganilwa
          Me
05
2010- 2015
Mhe. Peter P. Tweve
          Me
06
2016 Mpaka sasa
Mhe. Festo E. Mgina
          Me

Wahe. Wabunge Tangu Mwaka 1965 

Na.
Mwaka
              Jina
    Jinsi
01
1965 - 1967
Mhe. Gustav P. Mwinuka
     Me
02
1967 - 1970
Mhe. M.S Mwakigonja
     Me
03
1970 -1990
Mhe. J.J Mungai
     Me
04
1990- 1995
Mhe. William Mwagamalindo Mpiluka
     Me
05
1995- 2010
Mhe. J.J Mungai (Muf. Kas)
Mhe. Malangalila( Muf. Kus)
     Me
06
2010 Mpaka sasa
Mhe. Mahamoud Mgimwa( Muf. Kas
Mhe. Menradi  Kigola (Muf. Kus)
     Me
 
 
 
 
 
 
 
 

 Kuanza rasmi kwa Shughuli zake Kama Halmashauri Kamili Mwaka 1984

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi chini ya Sheria ya Madaraka Mikoani ya 1982 iliundwa Disemba 31 mwaka 1983 na ilianza rasmi shughuli zake tarehe 01 Januari 1984. Kabaada ya hapo shughuli za Halmashauri zilikuwa zinatekelezwa na Serikali kuu kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa (RDD)

 Wakurugenzi waliokuwepo kwa Vipindi tofauti.1984 - 2018

Na

   Mwaka

Jina

Jinsi

01

1984 -1986
Bwana. A.Z Mung’ong’o

Me

02

 1986-1991
Bwana. Mwambeso
               Me

03

1991 - 1994
Bwana. Collnel Kisege
                Me

04

1994- 1997
Bwana. William Kipigapasi

Me

05

1997- 2002
Bibi. Theresia Mmbando

Ke

06

2002-2007
Bwana. Halfan Halifa Hida

Me

07

2007- 2013
Bwana. L.E.S Shimwela

Me

08

2013 - 2015
Bwana P. Ntinika

Me

09

2015 - 2016
Bibi. Saada  I.   Malunde

Ke

10

2016- Mpaka sasa
Profesa. Riziki S. Shemdoe

Me

 

 

 

Tangazo

  • Tunakodisha Ukumbi wa Halmashauri Uliopo Mafinga April 17, 2017
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Bilioni 55 Kutumika Bajeti ya 2023/2024 Halmashauri ya Mufindi

    February 07, 2023
  • Mkuu wa Mkoa Aridhishwa

    December 13, 2022
  • Bilioni 1.4 za World Vision Kunufaisha Maelfu ya Kaya Mufind

    December 06, 2022
  • Watumishi Halmashauri ya Mufindi Waaswa Kuwa Wamoja na Kuzingatia Maadili ya Kazi

    November 25, 2022
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.