- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
-
Utawala
- Muundo wa Taasisi
-
Idara
- Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
- Idara ya Utumishi na Utawala
- Idara ya Fedha na Biashara
- Planing and Statistics Department
- Idara ya Elimu Sekondari
- Idara yaElimu ya Msingi
- Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
- Idara ya Afya
- Idara ya Maji
- Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
- Idara ya Mifugo na Uvuvi
- Idara ya Ujenzi
- Kitengo
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari


Shirika la LYRA limekabidhi bweni jipya katika Shule ya Sekondari Idunda, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ikiwa ni hatua kubwa ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuinua ufaulu wa wanafunzi wa kike, ambapo bweni hilo limejengwa kwa lengo la kupunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili wanafunzi wa kike waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufika shuleni hali iliyokuwa ikisababisha utoro na kushuka kwa ufaulu.
Akizindua bweni hilo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mh. Dkt. Linda Salekwa ameishukuru LYRA kwa mchango huo mkubwa na kuwataka walimu na wazazi kushirikiana kuhakikisha ndoto za wanafunzi wa kike na wa kiume zinatimia. huku akitoa onyo kali kwa walimu wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi ambapo amesema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kujihusisha kimapenzi na wanafunzi.

Aidha ametoa rai kwa wazazi na walezi kutoa ushirikano wa kutosha kwa bodi ya shule na walimu kwa kuwahakikisha wanashiriki kikamilifu katika malezi ya watoto watakaoishi bweni ikiwemo upatikanaji wa chakula huku akiwasihi walimu kusimamia na kuwa walezi wa watoto ili wapate elimu iliyokususdia badala ya kuwa sehemu ya ushawishi na kwamba mwalimu yoyote atakayebainika kuwa sehemu ya ushawishi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Lyra in Africa Bw. Gerald Usika amesema shirika hilo kwa kushirikiana na Jamii na Serikali limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule za sekondari za kata zilizopo mkoani Iringa kwa lengo la kusaidia kupunguza tatizo linalowakabili watoto wa kike, kuhakikisha kuwa wako salama na kuwa na uhakika wa kumaliza kidato cha nne salama. huku akisema kuwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi imefanikiwa kufikisha mabweni matano, mawili yakiwa katika Shule ya Sekondari Kihansi, Kata ya Mapanda. moja katika shule ya sekondari ya Maduma kata ya Maduma na Moja katika shule ya sekondari Ifwagi kata ya Ifwagi. 




Hafla hiyo ya makabidhiano ya bweni hilo iliambatana na matukio mbalimbali ikiwemo utiaji saini hati ya makabidhiano ya bweni, makabidhiano ya hati, ugawaji wa vyeti kwa wadau mbalimbali walishiriki katika kufanikisha ujenzi wa bweni pamoja na upandaji miti katika eneo la bweni.


