• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HAKIKISHENI MAREJESHO YANAFANYWA KWA MWITIKIO MKUBWA - DAS MUFINDI

Posted on: September 25th, 2025

Wanavikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu  waliopata mikopo ya 10% wametakiwa kuwa na mwitikio mkubwa wa kufanya marejesho ya mikopo hiyo kwani fedha hizo ni za mzunguko zinazopaswa kutumikwa kujikwamua na kurejeshwa kwa wakati ili ziweze kusaidia vikundi vingine kwa kuhakikisha kila kikundi kinajibidiisha na kutekeleza mradi wake kama ilivyokusudiwa.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala Wilaya Ndg. Reuben Chongolo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi ya kiasi cha shilingi 1,015,224,500.00 kwa vikundi hivyo ambapo amesisitiza marejesho kufanyika kwa wakati jambo litakalosaidia upatikanaji wa fedha nyingine kwa ajili ya vikundi vingine ambavyo vinahitaji kupatiwa mikopo ya 10% ili viweze kujikwamua kiuchumi.


Hafla hiyo iliyoambatana na ugawaji wa vipaza sauti kwa maafisa maendeleo ya jamii waliko kwenye kata ambapo vipasa sauuti 10 vimekabidhiwa kwa kata 10 ikiwa ni awamu ya kwanza ambapo amewasisitiza maafisa hao kutumia vitendea kazi hvyo kama ilivyokususduiwa na Serikali ikiwemo kuendelea kutoa elimu na ushauri wa kitaalam hususani kwa wanavikundi na wananchi katika uchaguzi wa maandiko ya miradi illi waweze kuchagua miradi inayotekelezeka jambo litakalosaidia usimamizi  na urejeshaji wa mikopo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambaye pia ni Afisa Maliasili Wilaya Ndg. Gilbert Ngailo amewataka wanavikundi waliopata mikopo kuzingatia taratibu na sheria katika uendeshaji wa kila mradi ulioainishwa ikiwemo kuhakikisha wanakuwa na leseni za uendeshaji biashara na umiliki wa vyombo vya moto huku akisisitiza urejeshaji wa marejesho ya mikopo hiyo kwani wana dhamana ya kurejesha.

Akisoma taarifa ya mikopo ya 10% Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Ndg. Sebastian Kaole amesema Halmashauri ya wilaya ya Mufindi imeendelea kuratibu Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake,Vijana na Watu Wenye Ulemavu kama sheria na kanuni zinavyoelekeza.kwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya makundi matatu ya vikundi vya wajasiriamali Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ambapo jumla ya shilingi 1,015,224,500.00 zimetolewa kwa vikundi 98, kati ya hivyo 48 vikiwa ni vya Wanawake, 38 vya Vijana na 12 vya Watu Wenye Ulemavu.

Kwa niaba ya wanavikundi wote Bi. Mgeni Kalinga ametoa shukrani kwa Serikali na uongozi mzima wa Halmashauri na Wilaya kiujumla kwa huku akiwakumbusha wanavikundi wenzake kuhakikisha wanajenga Imani kwa Serikali kwa kufanya marejesho kwa wakati illi waweze kuaminika na kukopesheka zaidi.

Tangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MUDA MAPATO MUFINDI DC SEPT 2025 September 24, 2025
  • TANGAZO LA KAZI ZA MUDA USAFI MUFINDI DC SEPT 2025 September 25, 2025
  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Lyra yapeleka neema ya bweni shule ya sekondari Idunda

    October 21, 2025
  • HAKIKISHENI MAREJESHO YANAFANYWA KWA MWITIKIO MKUBWA - DAS MUFINDI

    September 25, 2025
  • Ziara yenu ikazae mbinu mpya utekelezaji program ya ECO-SCHOOLS -Kaimu DED Mufindi DC

    September 22, 2025
  • Mufindi DC yajikita zaidi kupunguza vifo vitokanavyo na changamoto za uzazi

    July 14, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.