• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa Ametoa Siku 90 Wazee Wote Wawe Wamekabidhiwa Vitambulisho Vya Matibabu.

Posted on: August 16th, 2018

Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa Ametoa Siku 90 Wazee Wote Wawe Wamekabidhiwa Vitambulisho Vya Matibabu


Mkuu mpya wa Mkoa Iringa Mhe. Ally Hapi, ametoa Siku 90 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa, Kuhakikisha wazee wote Mkoani humo wanatambuliwa na   kupewa vitambulisho vya matibabu bure ili waweze kutibiwa kwenye hospitali yoyote ya umma bila usumbufu.


Mhe. Hapi, ameyasema hayo  wakati akizungumza na watumishi wa umma Wilayani Mufindi katika ziara yake ya kwanza yenye lengo la kujitambulisha kwa watumishi wa umma  Wilayani Mufindi.
“Na Kwenye hili nimesema wazee wasiwafuate Halmashauri kwenda kupewa hivyo vitambulisho bali Halmashauri Kupitia DMO na timu yake mtoke muwafuate wananchi kata kwa kata muwaandikishe, Muwaasajili na kisha muwapelekee vitambulisho mahali walipo na baada ya siku 90 nataka nipate mrejesho chanya kuhusu agizo hili”.


Akizungumzia suala  la utendaji kazi, Mhe. Hapi, amewataka watumishi kutofanya kazi kwa mazoea bali kutimiza wajibu wao kwa ubunifu na uaminifu kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria ili kuleta matokeo chanya kwa umma wanaoutumikia.


“Awamu ya tano inazungumzia hapa kazi tu, kwanza ni lazima mkiheshimu chama cha mapindizi maana serikali hii haikujileta yenyewe, pili, lazima watendaji mtoke ofsini na kwenda kuwahudumia wananchi ili kutatua shida zao, kutenda haki na kuwa waadilifu lakini pia  ni lazima tuongeze juhudi za kukusanya mapato ya serikali kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ili Halmashauri  zote za Mkoa wa Iringa zisishuke asilimia 90%”alisema Mhe Hapi. 


Katika hatua nyingine, Mhe. Hapi amesema anatarajia kuanza kufanya mikutano ambapo kwa muda wa siku 18 atazunguka kwenye Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa na kufanya mikutano isiyopungua mitatu  kwenye kila Tarafa katika mikutano hiyo, atazungumza na wananchi sanjari na kusikiliza kero zao zoezi ambalo litaitwa Iringa Mpya.


Akisoma taarifa ya Wilaya, Mkuu wa wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William, amesema, anaishukuru serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli, kwa kuendelea kuleta fedha katika Wilaya yake.


Ameongeza kuwa, mwaka 2017/2018 Wilaya ya Mufindi ilipokea fedha kutoka serikali kuu kiasi cha Tsh Bilioni 06 na Milioni 200 kwa ajili ya maendeleo na matumizi ya kawaida.

Tarehe 28 Julai Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimteua Mhe. Ally  Hapi, Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa akirithi nafasi ya Mhe. Amina  Masenza, aliyestaafu kwa mujibu wa sheria, awali Mhe.  Hapi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es alaam.

Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.