• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Milioni 400 kujenga na kukarabati Kituo cha Afya Malangali

Posted on: January 3rd, 2018

Milioni 400 kujenga na kukarabati Kituo cha Afya Malangali  Mufindi

 

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mufindi itatumia jumla ya shilingi Milioni Mianne (400) kujenga na kufanya ukarabati mkubwa wa kituo cha Afya Malangali, kilichopo kata ya Malangali Halmashauri ya Wilayani Mufindi, ikiwa ni mkakati wa Serikali kuimarisha sekta muhimu ya Afya hususani Afya ya Mama na Mtoto.

Ujenzi na ukarabati wa kituo hiki cha Afya, unaotarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa, unafanyika baada ya Ofisi ya Rais – Tamisemi, kutoa kiasi cha Shilingi Milioni mianne (400) kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya kituo hicho ili kiweze kukidhi haja ya kutoa huduma bora za Afya kwa zaidi ya Wananchi elfu arobaini na nane (48,000) wa Tarafa ya Malangali watakao pewa rufaa kutoka kwenye Zahanati za Vijiji.

Matumizi ya kiasi hicho cha fedha, ni pamoja na kujenga jengo la kisasa la Maabara, Nyumba ya Mganga, kukamilisha ujenzi unaoendelea wa chumba cha upasuaji sanjari na kufanya ukarabati mkubwa wa Wodi maalum ya wazazi / Mama na Mtoto.

Ujenzi na ukarabati wa kituo, utatekelezwa kwa mfumo wa (Force Account) ambapo, Halmashauri itatumia Mafundi wenyeji watakaothibitishwa kuwa na uwezo unaokubalika wa kutekeleza jukumu hili kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu, badala ya mtindo uliozoeleka wa kutumia Wakandarasi. Pia, ili kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika, Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji, imeunda Vikosi kazi vitatu (03) vikijumuisha Maofisa kutoka idara mbalimbali maalum kwa kuratibu na kusimamia mradi huu kwa kuzingatia wakati na ubora.

Aidha, kwa kuwa uboreshaji wa kituo hiki, utatekelezwa kwa mfumo wa (Force Account) kama ambavyo imefafanuliwa hapo juu, Mkurugenzi Mtendaji anawahamasisha wananchi wote wa Tarafa ya Malangali  kujitolea nguvu kazi pindi itakapohitajika wakati wa utekelezaji wa mradi huu kwa ustawi wa Afya ya kila mkazi wa Tarafa ya Malangali na Halmashauri ya Mufindi kwa ujumla.

Imetolewa na,

Ndimmyake Mwakapiso,

Ofisa Habari na Mawasiliano Halmashauri ya (W) Mufindi.

Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.