• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MHE. KIHENZILE APONGEZA JUHUDI ZA WADAU KATIKA KUMKOMBOA MTOTO WA KIKE

Posted on: July 4th, 2024

Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa Mufindi Kusini Mhe. David M. Kihenzile ametoa pongezi kwa shirika la SAWA Wanawake Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo kuhakikisha mtoto wa kike anafikia ndoto zake ambapo shirika hilo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limefanikisha ujenzi wa bweni kwa wanafunzi wakike katika shule ya Sekondari Kasanga katika kata ya Kasanga.

Mhe. Kihenzile ametoa pongezi hizo Juni 4, 2024 wakati wa hafla ya kuzindua bweni hilo ambapo ameupongeza uongozi wa SAWA, Uongozi wa Halmashauri  ya Wilaya ya Mufindi pamoja na wananchi kwa juhudi kubwa na ushirikiano waliounyesha katika kuhakikisha bweni hilo linakamilika na kuanza kutumika.

Bweni hilo lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 138 kwa michango toka kwa wadau mbalimbali ambapo shirika la SAWA kwa kushirikiana na Coastward Foundation wamechangia shilingi milioni 1.8, Halmashauri ya Mufindi milioni 20, nguvu za wananchi shilingi milioni 7.5 huku mbunge huyo akichangia shilingi milioni 2.4, ambapo kukamilika kwa bweni hilo kutaongeza ufaulu, kuwajengea mazingira na muda mzuri wa kujisomea pia litawasaidia wanafunzi wa kike kuondokana na mimba za utotoni.


Aidha Naibu Waziri huyo, ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi hususani Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi Mtendaji kwani wamekuwa ni viongozi wasikivu, mfano wa kuigwa na wenye ushirikiano katika kuhakikisha Halmashauri ya Mufindi inakuwa na maendeleo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ambaye ni Afisa Elimu Sekondari Ndg. Daniel Mapilya amewapongeza wadau na wananchi wa kata ya Kasanga kwa kujitoa kwao kwa hali na mali ili kukamilisha ujenzi huo huku akitaka bweni hilo kuanza kutumika ili kupata matokeo yenye tija.


Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ya Kasanga Mhe. Costa Ng’umbi kwa kushirikiana na Mkuu wa shule ya sekondari Kasanga Bi. Monica Ng’amilo wameshukuru kwa kukamilika kwa ujenzi huo na wamepongeza  jitihada zinazoendelea kutekelezwa na Serikali huku wanafunzi hao kwenye risala yao wamesema uwepo wa bweni hilo litawaepusha na changamoto mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni, utoro jambo linaloathiri maendeleo ya taaluma.

Tangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MUDA MAPATO MUFINDI DC SEPT 2025 September 24, 2025
  • TANGAZO LA KAZI ZA MUDA USAFI MUFINDI DC SEPT 2025 September 25, 2025
  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Lyra yapeleka neema ya bweni shule ya sekondari Idunda

    October 21, 2025
  • HAKIKISHENI MAREJESHO YANAFANYWA KWA MWITIKIO MKUBWA - DAS MUFINDI

    September 25, 2025
  • Ziara yenu ikazae mbinu mpya utekelezaji program ya ECO-SCHOOLS -Kaimu DED Mufindi DC

    September 22, 2025
  • Mufindi DC yajikita zaidi kupunguza vifo vitokanavyo na changamoto za uzazi

    July 14, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.