• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru arizishwa, ubora wa Miradi ya Halmashauri ya Mufindi

Posted on: May 24th, 2018

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru arizishwa,  ubora wa Miradi ya Halmashauri ya Mufindi

Jumla ya Miradi 06 yenye thamani ya shilingi bilioni 9.199 imezinduliwa, kuwekewa mawe ya msingi pamoja na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru, ulipokimbizwa katika Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi, huku wakimbiza Mwenge kitaifa wakiridhishwa  na viwango vya miradi husika na kutanabaisha kuwa vinaendana na thamani ya fedha zilizotumika.

 Ukiwa katika Halmashauri  ya Wilaya ya Mufindi  Mwenge wa Uhuru  umeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa   Sekondari  ya Igombavanu, umezindua klabu ya wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Igombavanu,  ujenzi wa zahanati ya Kijiji pamoja na kukagua mradi wa hifadhi ya mazingira katika msitu wa kupandwa wa Halmashauri  Kijiji cha Mtili,  umezindua ujenzi wa Barabara ya lami Kitiru- Itulituli yenye urefu wa Kilomita 14.972, na mradi wa kilimo na mifugo wa mwananchi  kata ya Igowole.

Akizungumza wakati wa kutoa ujumbe wa Mwenge,kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu. Charles Francis Kabeho, amewahamasisha wananchi kuwekeza katika elimu kwa  kugharamia mahitaji muhimu ya Watoto wao, kama mavazi, viatu, Madaftari  sanjari na kuchangia mchango wa Chakula cha mchana kwa wanafunzi wa kutwa  chini ya ujumbe mkuu wa mbio za Mwenge 2018 “ELimu ni Ufunguo wa Maisha Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu”

Aidha, ameendelea Kuhamasisha kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, VVU/UKIMWI, dawa za kulevya na mapambano dhidi ya Malaria.

“Maambukizi ya UKIMWI yameendelea kuwa tatizo kubwa katika Mkoa wa Iringa, mkiongozwa na Mkoa wa Njombe wenye asilimia 11.4, wakati ninyi mnashika nafasi ya pili kitaifa kwa kuwa na maambukizi ya asilimia 11.3 hivyo, inatupasa tuchukue hatua za kubadili tabia kwani hali hii ikiendelea hivi ni hatari kwa maendeleo ya Taifa’’ alisema Kabeho

Kwa Upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, Kupitia risala ya utii  kwa mkuu wa nchi, amemhakikishia  Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwamba, Wilaya yake, itaendelea kutekeleza  Maagizo mbalimbali ya Serikali ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa viwanda, usimamizi wa Mbolea ya ruzuku, kuokoa mifumo ya kiikolojia ya bonde la Mto ruaha mkuu pamoja  na suala la Waalimu Kutojihusisha na michango ya Wazazi Shuleni .

Mkesha wa Mwenge wa Uhuru uliambatana na zoezi la upimaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI na katika upimaji huo,  jumla ya watu 435 walijitokeza kujua Afya zao, kati yao wanaume ni 232 na Wanawake ni 203 ambapo katika zoezi hilo ni watu 04 tu ndio waligundulika kuwa na maabukizi ikiwa ni Wanawake 02 na Wanaume 02.

 

Tangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MUDA MAPATO MUFINDI DC SEPT 2025 September 24, 2025
  • TANGAZO LA KAZI ZA MUDA USAFI MUFINDI DC SEPT 2025 September 25, 2025
  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Lyra yapeleka neema ya bweni shule ya sekondari Idunda

    October 21, 2025
  • HAKIKISHENI MAREJESHO YANAFANYWA KWA MWITIKIO MKUBWA - DAS MUFINDI

    September 25, 2025
  • Ziara yenu ikazae mbinu mpya utekelezaji program ya ECO-SCHOOLS -Kaimu DED Mufindi DC

    September 22, 2025
  • Mufindi DC yajikita zaidi kupunguza vifo vitokanavyo na changamoto za uzazi

    July 14, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.