• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Waziri JAFO Awang'akia TBA Kwa Ukarabati Mbovu Malangali Sekondari, Aridhishwa ujenzi wa Kituo cha Afya chini ya Halmashauri Mufindi

Posted on: June 11th, 2018

Waziri  JAFO Awang'akia TBA Kwa Ukarabati Mbovu Malangali Sekondari, Aridhishwa Ujenzi wa Kituo cha Afya chini ya Halmashauri  Mufindi

Waziri wa  nchi Tawala  za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI ) Mhe. Selemani Jafo, amewaagiza wakala wa Majengo TBA Mkoani Iringa, kurudia ukarabati wa sakafu za madarasa ya Sekondari kongwe ya Malangali baada ya kubaini kuwa imejengwa chini ya kiwango, huku akipongeza ujenzi wa kituo cha Afya Malangali unaotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa mtindo wa ‘Force Account’

Waziri Jafo, ametoa agizo hizo wakati wa ziara  ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Malangali, baada ya Ofisi ya Rais TAMISEMI  kutoa shilingi milioni 400 za kutekeleza mradi huo.

Jafo, amesema yeye kama Waziri mwenye dhamana na Shule hapa nchini, hawezi kuvumilia anapoona Taasisi ya Serikali inatekeleza mradi chini ya ya kiwango wakati inalipwa mabilioni ya fedha za umma.

“Halafu mimi Jafo Shule zipo chini yangu unafikiri nitakubali “I never” ni bora mngeacha Sakafu ya kwanza, Taasisi ya Serikali ni lazima ifanye  kazi ya Serikali kiusahihi na si kiujanja ujanja kama hivi, nenda mkaone Majengo ya Kituo cha Afya hapo jirani yaliyojengwa kwa Force account, Majengo ni mazuri yanaubora chini yamewekwa “tiles” alisema Waziri huku akigonga viatu vyake kwenye sakafu ambayo ilionesha vyufa kadri alivyokuwa akigonga.

Akijibu hoja za Waziri, fundi Mkuu wa TBA katika mradi huo  Bi.Agnes Haule, amekili udhaifu wa ujenzi na kufafanua kuwa, sababu ya tatizo hilo linatokana na uamuzi wa kusakafia kabla ya kukauka kwa zege kutokana na uhitaji wa vyumba vya kusomea na kuongeza kuwa wapo tayari kurudia kazi hiyo.

Awali akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Malangali, unaotekelezwa kwa mfumo wa force account kwa kutumia mafundi wenyeji Mh. Jafo, amefarijika na maendeleo ya ujenzi huo kwa kuwa umezingatia viwango na thamani ya fedha.

“Kazi hii inamaanisha kwamba tunauongozi mzuri wa Halmashauri ya Mufindi na Wilaya nzima ya  Mufindi na hakikisheni mnamaliza kazi hii ikiwa salama, nimeangalia vitu mbalimbli, kuta zenu na ujenzi kwa ujumla mko vizuri. Aidha, mnavyofanya vizuri mnatushawishi zaidi kwamba siku nyingine tunapokuwa na mradi, tuifikirie Mufindi kwanza na haya ndiyo  mambo  ambayo Mheshimiwa Rais anataka kuyaona na si vinginevyo”

Mnamo mwezi wa 12/ 2017, Halmashauri ya Mufindi ilipokea kiasi cha shilingi milioni 400 kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ili zitumike kufanya utanuzi wa kituo cha Afya Malangali unaojumuisha, Nyumba ya Mganga, Maabara, Chumba cha upasuaji na Wodi ya Mama na Mtoto na ujenzi wake ulianza rasmi mwezi 01/2018 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu wa 06.

 



Waziri Jafo akikagua Jengo la Maabara, kituo cha Afya Malangali


Waziri Jafo akimsabahi kaimu Mkurugenzi wa Halamshauri Bw. Isaya Mbenje mara baada ya kuwasili katika 

viwanja vya kituo cha Afya Malangali.

Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Sioasa Mkoa yakoshwa utekelezaji miradi ya maendeleo Mufindi DC

    May 18, 2025
  • DC Salekwa apongeza baraza la madiwani kupitisha miradi kwa mapato yua ndani

    May 16, 2025
  • RC IRINGA AKAGUA MIRADI NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

    May 09, 2025
  • Baraza la Madiwani Halmashauri Wilaya ya Mufindi Lapitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti RUWASA na TARURA kwa mwaka wa fedha 2025/2026

    May 14, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.