• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Baraza la Madiwani Mufindi Laweka Mikakati Ya Kulitangaza Bwawa La Maajabu La Mpanga Tazara.

Posted on: February 4th, 2019

Baraza la Madiwani Mufindi Laweka Mikakati Ya Kulitangaza Bwawa La Maajabu La  Mpanga Tazara.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ,limepitisha azimio la  mpango mkakati wa kuongeza vyanzo vya   mapato kwa kukitangaza rasmi kivutio kikubwa na cha kipekee hapa duniani ambacho ni bwawa la maajabu la Mpanga Tazara lililopo kata ya Mpanga Tazara Halmashauri ya Mufindi ambalo linamaajabu ya kuwa na visiwa vinavyoelea juu ya maji na kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine  vikiwa na uoto wake wa asili

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe. Festo Mgina, ameridhia hoja hiyo baada ya  kuibuliwa na mjumbe wa baraza hilo Diwani wa kata ya Mdabulo Mhe. Ernei Nyeho, wakati akichangia hoja katika kikao cha baraza.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati sasa wa kuwa na mipango kabambe juu ya bwawa letu la Mpanga Tazara, tunatakiwa kutangaza majabu yaliyopo katika bwawa hili ili kuvutia watalii wengi na hatimaye kupata fedha kwa ajili ya Halmashauri hivyo kuchochea maendeleo” alisema Nyeho.

Kama ishara ya kukubaliana na Diwani huyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Festo Mgina, ameiagiza kamati ya fedha uongozi na mipango ishughulikie suala hilo na kuliweka katika Mpango mkakati wa Halmashauri pamoja na kuiagiza kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira kuanzisha mchakato huo kwa mujibu wa kanuni.

Aidha, Mhe Mgina amesema mkakati  wa kwanza  uwe ni kuimarisha barabara ili kuwe na urahisi wa kufika eneo hilo la maajabu ambalo kwa sasa  linafikika kirahisi kwa kutumia usafiri wa treni.

Katika hatua nyingine Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imepokea Watendaji wa kata 11 kutoka sekretalieti ya ajira katika utumishi wa umma, watendaji hawa wanatarajiwa kutatua chanagamoto ya upungufu wa watumishi wa kada hiyo katika ngazi ya kata baada ya kuondolewa kwa kundi kubwa la Watumishi wakati wa Sakata   la kihistoria  la vyeti feki.

Sehemu Waajiriwa wapya 11  wa kada ya watendaji wa Kata wakitambulishwa mbele ya Baraza


Mhe. Nyeho Diwani wa Kata ya Mpanga Tazara, akijenga hoja ya kuweka Mpango Mkakati wa kulitangaza

Bwawa la Mpanga Tazara na maajabu yake

Kaimu Mkurugenzi Wakili Agape Fue, akizungumza wakati wa kikao cha Baraza

Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.