• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Bilioni 1.4 za World Vision Kunufaisha Maelfu ya Kaya Mufind

Posted on: December 6th, 2022

Bilioni 1.4  za World Vision Kunufaisha Maelfu ya Kaya Mufindi

05/12/2022

Waziri wa mifugo na uvuvi nchini Mhe, Mashimba Ndaki, leo amezindua mradi wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4 ambazo pamoja na mambo mengine zitatumika kununua na kuwapatia wananchi 1,200 wa kata za Nyololo na Maduma, mifugo ambayo ni ng’ombe jike wenyemimba 300, ngurue 600 pamoja na kuku 4,000 mradi ambao unanuia kupambana na utapiamlo kwa Watoto pamoja na kuwainua wananchi wa kata hizo kiuchumi chini ya ufadhili wenye tija kutoka shirika la World Vision. 

Akizungumza na wakazi Kata hizo mbili, katika uwanja wa Ofisi ya kata Nyololo, Mhe. Waziri Ndaki, ametoa wito kwa wanachi kuzingatia ufugaji bora ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji na kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu sanjari na kuendelea kutoa ushirikiano kwa mfadhili World Vision katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi kwenye kata zao, ili lengo la kuondokana na tatizo la utapiamlo kwa Watoto pamoja na kuinua uchumi wa kaya litimie kadiri ya matarajio.

“Bajeti ijayo serikali itawajengea majosho mawili ambapo moja litajengwa kata ya Nyololo na lingine kata ya Maduma, lakini pia mwakani kwenye bajeti ijayo lazima tutajenga kituo kimoja cha kukusanya maziwa, mtaamua wenyewe, iwe hapa Nyololo au katikati ya Nyololo na Maduma, mahali ambapo wafugaji wote wanaweza kufika, mtachagua wenyewe, kwa hiyo tujenge kituo ili tuweze kuwasaidia muwe wafanyabiashara wafugaji”

Naye Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mhe. David Kehenzile, ameliomba shirika la World Vision kupanua oneo la mradi ili  kuzifikia kata nyingine za ukanda wa joto na kubainisha kuwa ukanda huu wakazi wake wanachangamoto za kiuchumi ukilinganisha na ukanda wa baridi hivyo, kufikiwa na mradi huu kutachangia ukanda wote kuinuka kiuchumi

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh .Saad Mtambule, amesema, watandelea kushirikiana na World Vision katika utekelezaji wa miradi yote wanayoitekeleza katika sekta za muhimu za Elimu, Afya, kilimo pamoja na mifugo.

Awali akisoma taarifa ya shirika Mkurugenzi mwandamizi World Vision Tanzani Dkt. Pasco Mayala, ameeleza kuwa, shabaha ya mradi ni kunufaisha watu wengi zaidi, kwani kila mnufaika aliyepata ng’ombe au ngurue kwa mujibu wa mkataba, atalazimika kumgawia mtu mwingine endapo ng’ombe atazaa ndama jike  lakini pia mnufaika wa nguruwe atampatia mtu mwingine vitoto viwili vya ngurue ambavyo ni dume na jike kwa uzao wa kwanza wa ngurue.

Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.