• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Wajasiriamali wadogo wadogo Mufindi wafundwa nidhamu ya matumizi ya fedha

Posted on: February 10th, 2025

Wajasiriamali wadogo wadogo wametakiwa kuwa na maamuzi sahihi katka sekta ya ujasiriamali maamuzi ambayo yatawasaidia kufanya biashara sahihi, kwani katika kutafuta mali kunahitaji ujasiri, maamuzi sahihi, matumizi sahihi ya fedha yaliyo katika mpango ili kuwasaidia kupata faida.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Ndg. Daniel Mapilya wakati wa Hafla fupi ya ugawaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo wadogo chini ya mpango wa kuwatambua, kuwasajili na kuwapatia vitambulisho wajasiriamali wadogo wadogo, ambapo amewataka kuwa makini katika matumizi ya kiwango cha fedha kinachoingia na kinachotoka, huku akisisitiza kiwango kinachotumika kuwa kidogo na kinachoingia kuwa kikubwa,sambamba na kutumia fedha ambazo ziko kwenye mpango wa matumizi badala ya kutumia fedha ambazo haziko kwenye mpango wa matumizi kwa kuacha matumizi yasiyo ya lazima na yanayozuilika.

Akitoa mafunzo ya matumizi ya fedha Meneja wa benki ya NMB Ndg. Focus Lubende amewashauri wajasiriamali hao kuongeza zaidi fursa za kujiajiri ambazo watarithisha vizazi vyao sambamba na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha hususani katika kuweka malengo sahihi na kuyasimamia, kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameunga mkono juhudi za Serikali katika kuwajali wananchi ambapo kwasasa benki hiyo imepewa dhamana na Serikali ya kuwakopesha wajasiriamali wadogo wadogo wilayani Mufindi kiasi cha shilingi milioni 100 fedha zitakazowasaidia katika kukuza uchumi wao.

Kwa upande wake Mratibu wa Dawati la Wajasiliamali Wadogo Wadogo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Ndg. Revocatus Mgaya amesema mpango wa kuwatambua na kuwasajili wajasiliamali wadogo umeanzishwa na Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ukisimamiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ukiwa na lengo la kuwatambua, kuwasajili na kuwapatia vitambulisho ili kuwasaidia katika upatikanaji wa fursa za kiuchumi ikiwemo upatikanaji wa mikopo kwa taasisi za kifedha, ambapo kwasasa halmashauri imezindua mpango huo kwa kata za Nyololo, Igowole, Ihowanza na  Malangali kwa wajasiliamali 65 kupatiwa vitambulisho kwa awamu ya kwanza, huku mchakato wa kuwatambua na kusajili wajasiliamali toka kata nyingine ukiendelea.

Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Baraza la Madiwani Halmashauri Wilaya ya Mufindi Lapitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti RUWASA na TARURA kwa mwaka wa fedha 2025/2026

    May 14, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.