• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI KUANZA UKARABATI MIUNDOMBINU YA BARABARA JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI

Posted on: August 21st, 2024

 

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mh. Exaud Silaoneka Kigahe, ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara za jimbo la Mufindi Kaskazini.

Pongezi hizo amezitoa tarehe 20/08/2024 wakati wa mahojiano na redio Mufindi FM na kusema ukarabati huo utakuwa wa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ni kuanzia Barabara ya Mtili - Ifwagi yenye urefu wa kilometa 14 inayotarajiwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 23 ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami.

Maboresho hayo yameanza kufuatia uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua kubwa za mara kwa mara na kusema kuwa awamu ya pili ya maboresho ya barabara itakua Mdabulo-Lulanda yenye urefu wa kilometa 16 na barabara ya Mafinga-Mgololo kufanyiwa maboresho ya mapitio ili kuwa na miundombinu inayoendana na mazingira.

Ameongeza kuwa ujenzi wa barabara hizo ni kwa ubora wa hali ya hewa na aina ya biashara za jimboni hapo, kwani fedha zaidi ya shilingi bilioni 100 zimetolewa kujenga miundombinu ya barabara na kuongeza huduma za mawasiliano, maji na umeme katika maeneo mbalimbali yenye upungufu kama Ikwea, Ihimbo na Ilondo.

Aidha Mh. Kigahe amewaasa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kushiriki kikamilifu katika utunzaji na matumizi ya miundombinu hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wilaya na kwa mtu mmoja mmoja, huku akiwataka kuwa wavumilivu na kuiamini Serikali ya awamu ya sita ili kupata maendeleo zaidi.

Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.