• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mradi wa Bilioni 1.8 kuondosha shida ya Maji Kata ya Mtwango

Posted on: January 15th, 2018

Mradi wa Bilioni 1.8 kuondosha shida ya  Maji Kata ya Mtwango


 Hatimaye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetiliana saini na Kampuni ya Siha Enterprises Limited, kutekeleza ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji Sawala, wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8, utakao wanufaisha wananchi wa Vijiji vine vya Kata ya Mtwango baada ya kuikosa huduma ya Maji safi na salama kwa miaka mingi.

Hafla ya kihistoria ya kusaini kandarasi hiyo ya miezi 12, imefanyika katika kijiji cha Sawala mbele ya viongozi wa Vijiji vinne vya Sawala, Mtwango, Lufuna na kibao vinavyotarajiwa kunufaika na huduma hii muhimu kwa uhai wa binadamu.

Akizungunza mara baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo, kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye pia ndiye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, amemtaka Mkandarasi huyo kutekeleza mradi huo kwa ubora, kukamilisha kwa wakati  kadri ya mkataba aliosaini bila kuongeza gharama na ameahidi kuufuatilia mradi huo kwa kila hatua ya ujenzi.

Mh. Jamhuri pia, amewataka wananchi wa kata ya Mtwango kumpa shirikiano Mkandarasi  katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mradi, huku akikemea tabia ya uwizi kwa Vijana watakaopata ajira kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa kata ya Mtwango.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. Festo Mgina, amesema Ofisi yake inaimani kubwa na Mkandarasi huyo na akamtaka aanze kutekeleza ujenzi wa mradi kwa wakati kwani shauku pekee ya watu wa Kata ya Mtwango, ni kupata huduma ya Maji baada ya Mkandarasi wa awali kushindwa kukukidhi shauku yao.

Ujenzi wa mradi wa Maji Sawala, utakelezwa na kampuni wa  Siha  Enterprises Limited na utasimamiwa na Ofisi ya Maji Mjini Iringa (Iruwasa), Ofisi ya Maji ya Katibu tawala Mkoa pamoja na Ofisi ya Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa muda usizidi miezi 12. Aidha, baadhi ya shughuli kubwa zinazotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Matenki manne  ya ujazo wa lita 450,000, kusambaza mabomba kwenye Vijiji husika pamoja na kujenga vituo 122 vya kukinga Maji.

Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.