• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkuu wa Wilaya Mufindi awataka Wazazi kuchangia Chakula Shuleni

Posted on: June 4th, 2018

Mkuu wa Wilaya Mufindi awataka Wazazi kuchangia Chakula Shuleni.

 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amewataka wazazi na walezi waendelee kuchangia chakula cha mchana kwa wanafunzi wa kutwa kwa shabaha ya kuinua kiwango cha ufaulu, kupunguza utoro pamoja na kuleta usawa miongoni mwao.

Akiongea na wananchi wa Igowole katika kilele cha wiki la kusoma  lililofanyika katika Viwanja vya shule ya Msingi Igowole iliyopo Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bwana Joseph Mchina, amewataka vingozi wa serikali za vijiji kuendelea kutekeleza mkakati wa utoaji wa chakula cha Mchana shuleni kwa kuwamasisha wazazi kuchangia kwa mujibu wa sera ya Elimu bila malipo.

Aidha, amewapongeza viongozi wa siasa ambao wamekuwa bega kwa bega katika kuelimisha jamii na wazazi kuhusu umuhimu wa utoaji wa chakula cha mchana shuleni.

 “Napenda kupongeza kata zote ambazo zinazotoa chakula cha mchana kwa wanafunzi shuleni, utoaji wa chakula cha mchana shuleni huleta usawa kati ya walionacho na wasionacho, huimarisha mahudhurio ya wanafunzi shuleni huongeza usikivu wa wanafunzi darasani na hutunza muda wa ratiba nzima ya shule” alisema Mchina

Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bwana Kennedy Bukagile, alisema Halmashauri ya Wilaya Mufindi imejiwekea mkakati mzuri wa kuwapatia wanafunzi chakula cha mchana ili kuimarisha usikivu  na mahudhurio shuleni,

 “wazazi wamejitoa kulima shamba la maharage na Mahindi lenye jumla ya hekari 294 kwa ajili ya chakula cha mchana kwa wanafunzi shuleni”                    

Afisa huyo mwenye dhamana ya Elimu, ameongeza kuwa, Idara yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamewezesha kamati za shule kujengewa uwezo wa uhamasishaji na pia kuwa na wahamasishaji jamii  wa masuala ya  elimu kwa kila shule, wakishirikiana na kamati za shule kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata chakula cha mchana jambo ambalo limesabisha kuongezeka kwa ufaulu sanjari na kushuka kwa takwimu za utoro.

Kwa upande mwingine Maadhimisho hayo yalienda sambamba na maonesho ya mabanda ya elimu na mashindano ya wanafunzi katika stadi za KKK, ambapo washindi wa shindano hilo walitangazwa na kupewa zawadi na Mgeni rasmi ambapo nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Mwanafunzi Anania Ng’umbi, darasa la pili wa Shule ya Msingi Igowole.

Aidha “kujua kusoma na kuandika ni haki ya kila mtu jambo hilo linamsaidia mtu kuwa na uwezo na njia yenye kumuwezesha kufanya maendeleo katika maisha yake pamoja na watu wengine”, Tamko la Shirika la UNESCO

Maadhimisho ya Wiki la Kusoma yanalenga kukuza na koungeza ari ya ushindani katika kujifunza stadi za msingi za kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) Ujumbe wa wiki la elimu mwaka huu ni Stadi za KKK ni Msingi wa Elimu, tuwekeze katika Elimu kuelekea Uchumi wa Viwanda  




Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.