• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Milioni 400 Kujenga, Kukarabati Kituo cha Afya Ifwagi Halmashauri ya Mufindi

Posted on: July 16th, 2018

Milioni 400 Kujenga, Kukarabati Kituo cha Afya Ifwagi Halmashauri ya Mufindi 

 

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi itatumia kiasi cha shilingi milioni 400 zilizotolewa na  Ofisi ya Rais -TAMISEMI,  kujenga na kufanya ukarabati mkubwa wa kituo cha Afya Ifwagi kilichopo Kata ya Ifwagi ikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati wa Serikali unaokusudia kuiimarisha sekta ya Afya hususani Afya ya Mama na Mtoto katika Halmashauri ya  Mufindi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na Diwani wa kata ya Mninga Mhe. Festo Mgina, amesema, fedha hizo zitatumika kukarabati na kufanya utanuzi wa Wodi ya Wazazi, ujenzi wa jengo la upasuaji, ujenzi wa Nyumba ya Mganga sanjari na Jengo la Maabara.

Mhe. Mgina, amebainisha kuwa ujenzi na ukarabati huo, utatekelezwa kwa mfumo wa  “Force Account” ambapo Halmashauri hutumia Mafundi wenyeji watakao thibitishwa kuwa na weledi unaokubalika huku wakitakiwa kutekeleza jukumu hilo kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu chini ya usimamizi wa karibu kutoka kwa Mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri

 “Nawahamasisha wananchi wote wa kata ya Ifwagi, kujitolea nguvu kazi wakati wa utekelezaji wa mradi huu muhimu kwa ustawi wa Afya zetu na Halmashauri ya Mufindi kwa ujumla” alisema Mhe.Mgina,

Aidha, ili kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa wakati na ubora uliokusudiwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe, akiwa ndiye mtendaji Mkuu, ameunda kamati maalum yenye vikosi kazi vitatu vinavyojumuisha  Maofisa kutoka idara mbalimbali pamoja na wananchi ili kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa wakati na  kuzingatia viwango elekezi.

Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa mwaka jana Ofisi ya Rais -TAMISEMI ilitoa kiasi kama hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa kituo cha Afya Malangali kilichopo kata ya Malangali  na tayari ujenzi wake umekamilika na kinachosubiriwa ni mapokezi ya vifaa tiba  vyenye thamani ya shilingi Milioni 300 kutoka bohari ya dawa (MSD)


Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.