• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mikopo Ya Milioni 352 Umetolewa Kwa Wanawake, Vijana na Walemavu Mufindi

Posted on: July 2nd, 2020


Mkopo wa Millioni 352,250,000.00 Umetolewa Kwa Wanawake, Vijana na Watu Wenyeulemavu Mufindi

“Mkopo mlioupata leo, ukatumike kwenye malengo husika hasa katika kuwakomboa kiuchumi, kwa kufanya hivyo mtaweza kurejesha na kutimiza malengo ya Serikali ya kuinua wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kutoka katika umaskini”

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mufindi Ndugu Servi Ndumbalo, alipokuwa akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Jamuhuri William, katika hafla fupi ya utoaji wa mikopo kwa vikundi 113 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Amesema, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetimiza malengo iliyojiwekea kwa kutoa mikopo asilimia miamoja, (100%) ikiwa ni malengo waliyojiwekea ya kutoa mkopo kiasi cha shilingi milioni 602,760,963.48/= kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kutoka katika mapato yake ya ndani. Hivyo ameupongeza uongozi wa Halmashauri, wataalamu kwa kufikia malengo waliyojiwekea.

Akitoa taarifa ya mikopo, Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu, Robert Sungura, amesema kuwa Kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetoa mikopo yenye thamani ya Sh.602,760,963.48/=  kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.  

”Ndugu mgeni rasm, Fedha hizi za mkopo zilitolewa katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ilitolewa kiasi cha Sh. 240,782,000.00 mwezi Januari, 2020 kwa mchanganuo ufuatao; Sh. 233,251,000/=zilitolewa kwa vikundi 78 vya wanawake vyenye jumla ya wanufaika 948, kiasi cha Sh. 91,031,000.00 zilitolewa kwa vikundi 29 vya vijana  vyenye wanufaika 212 (me 129 na  ke, 83) na kiasi cha sh. 7,500,000/= zilitolewa kwa vikundi 3 vya watu wenye ulemavu vyenye jumla ya wanufaika 28” alibainisha Mkuu huyo wa Idara.

 

Aidha, aliendelea kutanabaisha kuwa, Katika awamu ya pili, Juni 2020; kiasi cha sh. 352,250,000.00 kimetolewa kwa kuviwezesha vikundi vya wanawake vijana na watu wenye ulemavu ambapo kiasi cha sh. 164,850,000/= kimetolewa kwa vikundi 56 vya wanawake vyenye jumla ya wanufaika 532, kiasi cha sh. 164,100,000/= kimetolewa kwa vikundi 50 vya vijana vyenye jumla ya wanufaika 337 (me, 172na Ke 165) na kiasi cha sh. 23,300,000/=kwa vikundi 7 vya wanufaika 43 wenye ulemavu (me, 23 na Ke 20).

Hafla za Utoaji mkopo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri (Bomani) zimehudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Ndugu Jeswadi Ubisimbali, wataalam mbalimbali na wananchi wa Wilaya ya Mufindi.


Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.