• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAMATI YA USHAURI MIRADI YA MFUKO WA HIFADHI YA MILIMA YATEMBELEA MIRADI KATIKA VIJIJI VYA KIPANGA, IHIMBO, UHAFIWA NA UKAMI-MUFINDI

Posted on: April 11th, 2022

KAMATI YA USHAURI MIRADI YA MAZINGIRA YATEMBELEA MIRADI INAYOTEKELEZWA KATIKA VIJIJI VYA KIPANGA, IHIMBO,UHAFIWA NA UKAMI- MUFINDI

Kamati ya Ushauri Miradi  Inayofadhiliwa na mfuko wa hifadhi ya milima ya TAO  la mashariki wilaya ya Mufindi inayoomgozwa na Mwenyekiti Mheshimiwa Zakayo Kilyenyi ambae ni Diwani wa Kata ya Kibengu, imefanya ziara ya  kutembelea, kukagua na kushauri kuhusu Miradi inayotekelezwa katika Kata za Mapanda na Kibengu katika vijiji vinne.

Vijiji vinne vinavyotekeleza Miradi wa Hifadhi ya Milima ya Tao la Mashariki ni vijiji vya Kipanga,Ihimbo, Uhafiwa na Kijiji cha Ukami.

Akisoma taarifa ya Utangulizi Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili ndugu Ubisimbali Jeswald amesema  kila kijiji kinatekeleza Miradi mitatu ya  Ufugaji wa Nyuki, Mradi wa upandaji wa miti ya Mbao na mradi wa uapandaji miti ya matunda.

Akizungumza  na vikundi vinavyotekeleza miradi hiyo Mjumbe wa Kamati ya Ushauri Miradi ya Mazingira Tao la Mashariki Mheshimiwa Festo Mgina ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi amesema  miradi hii ikitumiwa vizuri itazidi kupandisha Uchumi wa wananchi wa Kata hizo.

Pia amewashauri kuacha kuuza ardhi bila utaratibu kwani ardhi hiyo inarutuba ya kutosha ni mali ikitunzwa vizuri na miradi inakuja kwa wingi kwakuwa wameonyeaha uaminifu katika matumizi ya fedha wanazopewa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Wakitoa taarifa yao wanavikundi wanaotekeleza miradi hiyo wamesema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ubovu wa barabara kipindi cha Mvua inayopelekea  kuzolotesha ukuaji wa kiuchumi.

Wanavikundi hao wamejiwekea mkakati kuwa ifikapo mwaka 2024 kila kaya katika vijiji hivyo ihakikishe inakuwa na miche 20 ya zao la parachichi, pia wameomba Uongozi wa Halmashauri ya  wilaya ya Mufindi kuwawezesha badala ya kuletewe miche ya miti ya matunda basi waanzishe vitalu vya miche ya zao la Miti na Matunda katika maeneo yao wenyewe.

Akitoa kauli ya serikali kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Ndugu Ubisimbali Jeswald amesema kwa mwaka wa fedha ujao wananchi kwenye vijiji vyote vya mradi, watapata mafunzo ya kuanzisha bustani za miti ya matunda kwani andiko limeandaliwa na kupitishwa na TAO mashariki.

Ziara hiyo imehudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Ushauri Tao la Mashariki kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambao ni Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani na baadhi ya wataalamu .


Imeandaliwa na

Ofisi ya Habari na Mawasiliano

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

Afisa Habari

Sima Bingileki

Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.