• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Mufindi District Council
Mufindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Planing and Statistics Department
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara yaElimu ya Msingi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia na Vijana
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Tehama
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Kisheria
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na MH. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Taarifa
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DC Mufindi Aagiza Kusitishwa Kwa Huduma ya Maji Kata ya Mbalamaziwa

Posted on: April 5th, 2019


       DC Mufindi Aagiza Kusitishwa Kwa Huduma ya Maji Kata ya Mbalamaziwa

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, ameagiza kusitishwa kwa huduma ya Maji kwa wananchi zaidi ya 70 wa Kata ya Mbalamaziwa, waliojiunganishia Maji pasipo kufuata taratibu.

Kiongozi huyo Mkuu katika ngazi ya Wilaya ametoa agizo hilo katika Kijiji cha Nyanyembe kilichopo kata ya Mbalamaziwa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

“Wale wote walijiunganishia Maji kinyume cha utaratibu, natoa agizo, kuanzia leo Maji hayo yakatwe mara moja, lakini vilevile ipigwe hesabu tangu walipojiunganishia ili tujue wametumi Maji ya bure kiasi gani, walipe na yeyote atakayekaidi apelekwe Mahakamani” alisisitiza Mkuu wa Wilaya

Sanjari na hilo Mhe. William, imeitaka jumuiya ya watumia Maji COWSO katika kata hiyo, kuhakikisha  kila mwananchi anayepata huduma ya Maji  anailipia jambo ambalo litaiwezesha jumuiya  kukusanya Fedha nyingi zaidi hivyo kuwa na uwezo wa kupeleka   Maji kwa wananchi wengine ambao bado hawajafikiwa na huduma hiyo muhimu kwa uhai wa binadamu.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ametoa siku 60 kwa watu waliovamia chanzo cha Maji cha Nzivi, wawe wameondoka kwa hiari  kwenye  eneo hilo na endapo watakaidi kutekeleza agizo hilo, wataondolewa kwa nguvu ikiwa ni pamoja na kufunguliwa mashitaka.

Ukaguzi huo ulifanyika katika Kijiji cha Nyanyembe Kijiji ambacho kinatajwa kama Kijiji cha mfano kati ya vijiji 121 vya Halmashauri kwa usafi wa mazingira hususani matumizi ya choo bora.

Aidha, katika mashindano ya mwaka jana Kijiji cha Nyanyembe kilishika nafasi ya 07 kwenye mashindano ya usafi wa Mazingira na matumizi ya choo bora kati ya Vijiji vyote hapa nchini.










Tangazo

  • ORODHA-YA-ASASI-ZILIZOPATA-KIBALI-CHA-UANGALIZI-WA-UBORESHAJI-WA-DAFTARI-MWAKA-2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA KAZI JULAI 2024 MUFINDI DC July 22, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MUFINDI DC OKTOBA 2024 October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% MUFINDI DC October 02, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watendaji wa Kata na Vijiji wanolewa ukusanyaji wa kodi ya Majengo

    April 10, 2025
  • Watendaji wa kata wasisitizwa kuendelea kusimamia suala la lishe kwenye maeneo yao

    March 27, 2025
  • Watumiaji wa mfumo wa NeST wapigwa msasa Mufindi DC

    March 11, 2025
  • Milioni 758 kutekeleza miradi ya usafi na mazingira katika sekta ya afya na elimu

    March 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

MAKALA TASAF MUFINDI KAYA MASKINI
Video Nyingine

Viungio vya Haraka

  • Muongozo wa Kutumia Mfuo wa FFRAS

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Ajira za Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Iringa
  • Hati ya Mishahara ya Watumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://thesiswritingservice.net/

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mufindi District Council Office

    Postal Address: 223 Mafinga

    Telephone: 026 - 2772614

    Mobile: 026 - 2772614

    Barua Pepe: ded@mufindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani

Copyright ©2018 Mufindi District Council. All rights reserved.